Ad Code

Responsive Advertisement

Mbwana kusalia ligi kuu ya England

UK Premierleague Samatta (AFP/P. Ellis)
Mbwana Samatta ataendelea kuwika kwenye ligi kuu ya England katika msimu ujao baada ya timu yake ya Aston Villa kuponea chupuchupu kushuka daraja.
Mbwana Samatta ataendelea kuwika kwenye ligi kuu ya England katika msimu ujao baada ya timu yake ya Aston Villa kuponea chupuchupu kushuka daraja kufuatia sare ya 1-1 na West Ham katika mechi ya mwisho ya msimu wa ligi kuu ya England, PL.
Jack Grealish ndiye aliyeifungia klabu hiyo bao la pekee lililoinusuru Villa kushuka daraja kwa tofauti ya pointi moja tu. Bao hilo la Grealish kwa Aston Villa, ambayo ni klabu yake ya utotoni, huenda likawa la mwisho kufuatia fununu za kutaka kuihama baada ya msimu huu kumalizika. Hata hivyo bado haijawa wazi kuhusu hilo.
Kwa muda mrefu Villa ilikuwa miongoni mwa timu tatu zinazoshika mkia, na ilifanikiwa kutoka  kwenye kundi hilo baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Arsenal wiki iliyopita. Villa sasa itakuwa inashiriki ligi kuu kwa mara ya pili mfululizo.
Reactions

Post a Comment

0 Comments