Ad Code

Responsive Advertisement

MSIBA WA MKAPA: Kagame atangaza siku tatu za maombolezo




Rais wa Rwanda, Paul Kagame ametangaza siku 3 za maombolezo kuanzia leo hadi Julai 29 kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, Benjamin William Mkapa (81). 

Kagame ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) amemzungumzia Rais Mstaafu Mkapa kama kiongozi ambaye mchango wake ulienda nje ya mipaka ya Tanzania.

Rwanda inaungana na Watanzania kuomboleza kifo hicho na bendera za nchi hiyo pamoja na ile ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zitapepea nusu mlingoti.

Reactions

Post a Comment

0 Comments