
Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA) imeweka hatua za usajiliwa ndege zisizo na rubani (Drones) ili kudhibiti uhalifu ambao awali Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP David Misime alisema ndege hizo zisiposajiliwa zinaweza kutumika kwa nia ovu ili kuihujumu nchi.
Mbali na ndege hizo kutakiwa kusajiliwa kwa dola 100 (Tsh. 232,000) kwa mwaka usajili ambao utaruhusu ndege hizo kufanya kazi kimkoa, ndege hizo zinatakiwa kuwa na kibali kila mara inapotakiwa kufanya kazi.
Kibali cha Matumizi kitatolewa bila malipo kwa mtu mwenye Usajili, mbali na kibali, mtumiaji anapaswa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi na serikali ya mtaa wa eneo analotaka kufanyia kazi.
Aidha watumiaji wametakiwa kutumia ndege kulingana na usajili. Kila mtumiaji anapaswa kuainisha eneo la kazi, kazi yenyewe na muda wa kazi ili kupewa kibali cha kupata kibali cha kazi, ambayo itasaidia TCAA kufuatilia mahali ilipo ndege hiyo.


0 Comments