Ad Code

Responsive Advertisement

Biashara ya Usafirishaji kwa Bajaji: Ueandeshaji, Changamoto, Faida na Ushauri

 MAMBO YA MUHIMU KUZINGATIA 

Hii biashara ni nzuri lakini ina changamoto zake kama zilivyo biashara nyingine. Kwa kifupi nikupa yale machache ambayo ni ya kuzingatia katika hii biashara.

1. Hakikisha chombo kinalala kwako, maana usipofanya hivyo madereva wa bajaj wana kawaida ya kukifanyisha chombo kazi kwa muda wa saa zote 24 za siku kwa utaratibu wa kuwaachia deiwaka. Halafu wewe anakuletea Tsh 15000 tu, wakati unaweza kukuta wametengeneza hadi Tsh 70,000 (Kama siku ikiwa nzuri sana) kwa siku.

2. Hakikisha unasimamia service na uwe na rekodi ya siku unayofanya service maana usipofanya hivyo, kuna uwezekano ukaambiwa kuna service imefanyika ilipe utoe hela wakati hakuna kilichofanyika. Hii inaweza kufanya chombo kikachoka haraka hadi ukashangazwa.

3. Kama huna utaalamu hata kidogo na mambo vyombo vya moto, sikushauri hata kidogo kununua bajaj zilizotumika maana utatumia hela nyingi sana kulipa mafundi na kununua spea. Ni vizuri ununue vyombo vipya na pia usikae navyo sana, fanyia kazi si kwa zaidi ya miaka miwili, uza na ununue vingine.

UNAWEZA SOMA NA HII>>>Tabia za hovyo kwenye biashara

4. Usiwachekee kabisa hao madereva kwenye masuala ya hesabu maana hawachelewi kukuletea stori za biashara mbaya wakati wakipiga hela hawakuongezi hata sh 100 kwenye hesabu yako. Kama biashara mbaya weka deni, siku zijazo wajazie hiyo hesabu.


MAONI
UZOEFU WANGU

Mimi nafanya hiyo biashara, na mpk sasa ninazo mbili! inalipa sana hapa town ila kwa njia ya mkataba otherwise itakutesa kama huyo mkuu hapo aliyekua anachukua 15 kwa siku!

Ni hivi: mkataba huwa ni miez kumi na 8 (mwaka na nusu) na kwa siku kipande ni elfu 20 na anakupa kwa wik = laki na 40/- kwa mwez ( x 4 = 560,000/-) kwa mwaka na nusu itakua 560,000 x 18 = tshs 10080000/-

Kuhusu matengenezo huduma zote za kawaida anafanya dereva icpokua huduma kubwa kubwa tu ndo utahusika tena kwa kushea gharama na dereva!

Kuhusu ipi ni bora' kwa mkataba bora piagio siyo TVS

Kwann piagio? Kwasababu inanafas kubwa ya abiria kukaa na mizigo pia ukilinganisha na TVS
Tvs ni nzuri kwa mtu anaefanya biashara bila mkataba kwasababu ikimrudishia hela ni rahis kuiuza (inauzika kirahis/inasoko kubwa) na hii ni kwasababu ziliwah kuingia hapa bongo kabla ya piagio)

Uimara wa chombo uko mikonon mwa dereva! ila piagio sina shaka nazo kwenye uimara!

Nin faida ya kuingia mkataba?

1/ Bajaj haihitaj uangaliz mkubwa kwasabab dereva anajua baada ya miez kumi na 8 bajaj ni yake! ( hawez kuitumia roughLy)

2/ Ni win-win project yaan wote wanufaika dereva na boss pia hivyo bas haitakua kaz ngumu kumpata dereva

3/ Huduma za mara kwa mara hazitakuepo mana anakua anaiendesha kwa uangalifu mfano, hata *dei waka huwa hawatoi hawa madereva wa mikataba na kama ikitokea service anamaliza mwenyewe unLess iwe kubwa na pia mtashea gharama!

4/ Payback period ni kubwa kwa muda mfupi..

ANGALIZO>> usisahau kukatia BIMA bajaj yako tena BIMA kubwa! ili uondokane na stress inapokua barabarani!



NI BIASHARA YENYE FAIDA

Nakushauri ufanye hiyo biashara kwa kuwa ni profitable. Mimi pia ninafanya hiyo biashara na mpaka sasa ninazo mbili. Three-wheeler nzuri ni TVS King maana inadumu kwa muda mrefu na pia ni rahisi kupata spare zake na bei nafuu ukilinganisha na aina nyingine za Three-wheelers.

Mimi 'Bajaj' zangu kwa siku hesabu ni sh 20,000 each so kwa mwezi inanipa sh 600,000 kwa kila moja (hapo excluding services). Bajaj kwa mwezi zinafanya service mara mbili ili ziendelee kuwa na hali nzuri na esttimation ya service ni sh 22,000 so kwa mwezi gharama inakuwa sh 44,000-45,000.

Hakikisha unakuwa na kijana anayeeleweka maana huyu ndio a 'secret' ya mafanikio yako, chukua kijana mwenye 'commitment' hapo hutapata usumbufu sana. Pia hakikisha Bajaj yako ina vibali vyote ili usiwe unapoteza hesabu yako kwa kudanganya kuwa amekamatwa na traffic imebidi ampe hesabu yako, vibali ni SUMATRA, Insurance na Road licence (Road licence unalipia once tu maana serikali imetoa msamaha kwa Bajaj na pikipiki kwenye hili). I hope nimeweza kukusaidia kwa kiasi chake.

P.S Sehemu nyingine, mfano Africana njia ya chini hesabu ni sh 25,000 kwa siku so inategemea na location pia mkuu.


AINA ZA BAJAJI, CHANGAMOTO NA USHAURI

1. Naomba kufahamu bei halisi ya kununua bajaji mpya.

TVS-7.3M na RE BAJAJ-7M
2. Tahadhar muhimu za kuchukua/kuzngatia pindi naponunua bajaji mpya.
- Nunua mpya usichukue second hand
Umesema unatokea Mwanza, kwa jiografia ya huo mji chukua RE-BAJAJ hizi zina nguvu lakini sio fuel efficiency, spare parts zake ni ghali compared to TVS KING

3. Naomba kufahamu taratibu muhimu za kufuata kabla ya kuanza biashara hii.
- Tafuta dereva mzuri, huyu kumpata unaweza fanya uchunguzi kupitia watu wanaoendesha naye
- Ikatie comprehensive insuarance tumia bima ya CRDB ni 6% ya bei ya chombo
- Itengee akaunti special hela itakapokuwa inaingia

4. Changamoto za biashara hii
- Uaminifu wa madereva(hesabu)
Ajali barabarani
- Service on time kufanya
- Matumizi ya spare original

6. Ushaur kuhusu mengineyo
- Hakikisha unachukua hela kwa siku, usikubali uchukue hela kwa week mtasumbuana na dereva
- Siku ya service hakikisha unakuwepo wewe/muwakilishi kujiridhisha vifaa vinavyowekwa ni Genuine
- Kuna makampuni yana jishughulisha na kufanya service, usipende sana mafundi wa mitaani kuibiwa njenje
- mzuie/muonye dereva kukitoa chombo kukoroga/day waka

- Ukinunua chombo waweza kaa nacho miezi hata 6-8 then kitoe kwa dereva kama mkataba ili kisikusumbue saana 

Reactions

Post a Comment

1 Comments

Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)