Ad Code

Responsive Advertisement

76 Wafa Kwenye Mlipuko wa Bomu Mogadishu



BOMU la kutegwa ndani ya gari limelipuka leo asubuhi katika kituo kimoja cha ukaguzi wa usalama chenye shughuli nyingi katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, na kuwaua karibu watu 76

Mkuu wa hospitali ya Medina, Mohamed Yusuf, amethibitisha idadi hiyo akisema watu wengine 70 wamejeruhiwa.
Awali, msemaji wa serikali, Ismail Mukhta,r alisema idadi hiyo huenda ikaongezeka kwa sababu zaidi ya watu 60 wamekimbizwa katika hospitali mbalimbali.

Shambulizi hilo limekuwa moja ya mashambulizi mabaya zaidi kutokea katika siku za karibuni mjini Mogadishu.
Kapteni Mohamed Hussein amesema mlipuko huo ulikilenga kituo cha kukusanya kodi wakati wa pilikapilika za asubuhi kipindi wakazi wa neo hilo wakirejea kazini baada ya mapumziko ya mwishoni mwa juma.
Hakujatolewa taarifa yoyote kuhusu aliyehusika na shambulizi hilo. Kundi la itikadi kali la Al-Shabaab lenye mafungamano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda aghalabu hufanya mashambulizi ya aina hiyo.
Reactions