Ad Code

Responsive Advertisement

Aliyemuua mkewe kwa kumkata na shoka kusakwa na mabomu ya machozi




Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shanna amesema Jeshi hilo litatumia njia mbalimbali ikiwenmo Mabomu ya machozi kumsaka kijana  Latiaeli Pallangyo (28) ambaye anatuhumiwa kwa kumuua mpenzi wake Marry Richard kwa kumkata na shoka.



Disemba  25, 2019 muda wa saa 4 asubuhi, huko katika kijiji cha Kiringa, Wilaya ya Arumeru Marry D/O Richard Mushi (24) mkazi wa kijiji hicho, aiuawa kwa kakatwa na shoka kichwani na mwanaume aliyekuwa akiishi naye aitwaye Moses S/O Latiaeli Pallangyo (28) kwa jina maarufu Moses Lebaba anayejishughulisha na nyimbo za injili.

Akizunguza na waandishi wa habari jijini Arusha RPC Shanna amesema "chanzo cha tukio hili ni ugomvi wa kifamilia baina ya wawili hao. Mtuhumiwa alitoroka mara baada ya kufanya tukio hilo na tayari tumeanza kufanya msako mkali wa kumtafuta kwa kushirikna na vyombo vingine vya dola. Tunawaomba wananchi kuwa watulivu na wale wenye taarifa kuhusiana na tukio hili wasisite kutoa ushirikiano."

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya rufaa Mount Meru kwa uchunguzi zaidi wa Daktari.

"Pia nichukue fursa hii kuwapa taarifa fupi ya hali ya usalama Mkoa wa Arusha kwa kipindi hiki cha sikukuu ambapo mpaka kufikia hivi sasa hali ni shwari. Hakuna matukio makubwa ya kihalifu yaliyoripotiwa kwa Jeshi la Polisi Mkoani hapa. Niwahakikishie kuwa bado tupo imara kuhakikisha Sikukuu hizi za Mwisho wa mwaka zinasherehekewa kwa amani na utulivu." amesema Kamanda Shanna
Reactions