Ad Code

Responsive Advertisement

Anywabmaji ya Betri kisa Mapenzi


Mkazi mmoja wa Sanya Juu Katika Wilaya ya Siha, Godlisten Godson mwenye umri wa miaka 35 anadaiwa kujiua kwa kunywa maji ya betri huku ikidhaniwa kuwa chanzo ni migogoro ya kimapenzi kati yake na Mkewe.

Majirani wanadai kabla ya kuchukua uamuzi huo kulikuwa na ugomvi wa muda mrefu kati ya Godlisten na Mkewe chanzo kikiwa ni madai ya Mwanamke kumfuatilia Mumewe kwa hisia kuwa sio Mwaminifu.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Sanya juu Wema Gasino amethibitisha taarifa za kifo huku akisema hivi karibuni Mjomba wa Marehemu Godlisten alizikwa pia baada ya kujiua kwa madai ya kunywa maji ya betri.

“Nilienda kununua maziwa ili nipike chai niliporudi nikaambiwa Mume wangu amekunywa maji ya betri na kukimbizwa Hospitali ya Wilaya na alifia uko”- MKE WA MAREHEMU
Reactions