Ad Code

Responsive Advertisement

MJADALA: Biashara ya Madini ya Dhahabu: Fahamu Uwekezaji Wake, Changamoto na Faida

MTIRIRIKO WA NAMNA UNAVYOWEZA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HII

Hii biashara inakuhitaji sana mwenyewe uwepo eneo la tukio na uwe na akili nzuri kidogo ili kurun show na kutoboa.
Ni biashara nzuri kama kichwa chako ni kizuri na kweli una kiu ya mafanikio.

Kuna namna tofauti tofauti ya kujihusisha na hii biashara kwa mzoefu na kwa ambaye sio mzoefu.

Unaweza kufuata huu mtiririko kadiri uonavyoona inafaa.
  • Jipe muda kwa kuzungukia maeneo kadhaa ya uchimbaji ukiangalia nini kinachofanyika na namna gani watu wanaishi.
  • Kwenye mzunguko wako jipe muda sana kwenye machimbo mapya ya dhahabu.
  • Jaribu kuunda urafiki na watu wawili watatu watatu wanaofanya vitu vifuatavyo, mchimbaji, muuzaji, msagaji, mama ntilie, wenye mabaa na grocery ( tembelea hayo maeneo ujifunze kitu.)
  • Kwa wewe unayeanza sio jambo jema kuanza kununua na kuuza dhahabu kabla hujajua abcd za dhahabu - NI HATARI.
  • Ukiwa kwenye harakati za kusoma mazingira jiridhishe na biashara zote zisizo za dhahabu zinazofanyika na ambazo unaweza kuzifanya ili ukaishi mazingira hayo wakati unajifunza game.( kukodisha pump, blower, kuuza miti, mama ntilie, kuuza maji, grocery nk.
  • Ukipata kauzoefu kidogo Tafuta karasha la kusaga mawe used lenye hali nzuri kwa 5mil (jipya size ya kati ni 8.5 - 9 Mil).
  • Ukiwa na karasha fungua sehemu ya kusagia na kuosha (Mwalo) unapaswa kuwa na Karasha, mercury, mizani, magunia, maturubai ( roughly uwe na kama 10mil kibisha unaweza kuanza na 3mil nyingine iwe pembeni na total ni 13mil).
  • Wakati wa kusagisha na kuosha huwa unatarget vitu viwili ( Kuwa na rundo la mchanga hakikisha unasaga mawe yanayosoma vizuri na ununuzi wa dhahabu).
  • Hapo sasa ukiwa na mwalo na watu wanaoshea kwako unaweza kununua dhahabu kulingana na mzunguko lakini ukikomaa per day unaweza kulaza faida ya 100K +.
  • Ndani ya miezi sita mpaka mwaka kulingana na speed na usomaji wa rundo(kifusi) unaweza kuuza hela nyingi sana na ukatengeneza faida ambayo sasa ndio itakupa kiburi na kukubatiza kuwa miner sasa.
  • Mtaji ukikua sasa na bila shaka utakuwa unaijua network na dhahabu unaijua unaweza kuamua mwenyewe wakati unaendelea na karasha what is the next round..( Uanze uchimbaji [hii ni kamari na inahitaji ujasiri, hela na uwe mshirikina}, Ujenge plant kama mtaji umekua vizuri.
  • Binafsi sishauri sana kuingia kwenye uchimbaji unless uwe na muscles uchimbe kisasa kwa maana ya exploration na drilling ya kisasa otherwise hapo kuna mitihani sana na uamue kuikabili ( I know it and I'm doing this is reality, African magic is highly working here asikudanye mtu).
  • Kama uko vizuri na una muscles unaweza kujenga plant au ukanunua macompressor ukaanza kufanya drilling and blast kwa kukodisha.
  • Plant unaweza kuozesha mzigo wako mwenyewe unaosaga ukifikia kifusi cha kutosha na kukodisha pia wakati mwingine.
  • Unaweza usifanye shughuli yeyote ukamiliki plant ukawa unakodisha watu wanaozesha (usijiingize kwenye dhambi hapa kwa kuwapiga watu dhahabu plant kiujanja si jambo zuri kwa mpambanaji)
  • Gharama ya plant na kila kitu roughly 40mil to 50 mil.
  • Narudia tena, usifanye biashara ya dhahabu kabla hujaijua dhahabu NI HATARI, Usiwe na tamaa utatamanishwa utaingia king watu watakupiga, Usiwe na haraka jiwekee focus yako mdogomdogo utatoboa.
TAHADHARI: KAMA HUJUI DHAHABU UNAWEZA KUUZIWA FEKI

Kama huzijui unauziwa kitu fake. Kuna dhahbu hichafuka tu. Kwasababi ya mwamba kule chini au mercury kuwa chafu. Sasa ukinunua kwa bei elekezo utazika hela yako. Dhahabu chafu ina bei yake, maana had ioshwe na acid. Mambo mengi tu unapigwa huku jua linawaka!

Na upigaji mwingine uko jikonwakt wanachoma, so ni bora kucjomea jiko moja kuliko kuhama hama..kuna majiko kila unapopeleka mzigl wanawez kukuibia had point 8!..na huki ikichoma inabid ipungue kias kidg mayb .3(approx point 3)! Sasa hizl point 5 walizoiba ni approx 50000! Imagine uibiwe j3 had j3!

Hapo ndo mtaji unapokata!.kuchoma dhahabu lazima point fulani zipungue. Sababu ni nyinge esp kama haikuchomwa vizuri bado ina mercury...na jinsi ya kupma purity pale unaweza lia...unahakakika hii dhahabu safi na unajua hia zinasoma range hii had hii(mf, 80-87!) Majibu yanakuletea inasoma 78! Ikisoma hivuo unauza kwa hyo hyo bei78!labda wakuonee huruma wakununulie kwa 80!

Mambo ni mengi..ila ukipata chocho la kununua kwa bei elekez ukaenda uza kwa bei ya dunia uhakika wa kumake zaido ya lak 3 @ upo mkubwa! Tatizo connection, lakin ukisema ufate process ukate kodi hizi mpya mpya hapana...utaishia faida za 40000/-90000/= daily! Kama niko wrong wengine mtarekebisha!

SHUGHULI ZA MGODINI KWA WASIO NA MTAJI

Kiukweli kule ujitoe tu ufahamu kama huna mtaji! Kazi zipo ila za kutumia nguvu especially kuosha unga, kuchenjua dhahabu (hapa lazima ujifunze kwwli kweli) na ni ngumu mtu kukupa tope lake umchenjulie, wanaiba sana hapa kwa kuchenjua.

Kazi nazoona wanafanya zaidi kina kaka wasio na .mtaji ni kupiga moko(kuzamaa huko chini kupiga mwamba) ni kazk ngumu kiukweli, ila ukibahatika ukatoka na kajiwe uongo! Mistake za kule ni zile zile kwasababu kazi ni ngumu bas mtu akipata hela anatumia hovyo sana!

Kuosha unga ni 2000@ mzunguko mmoja. Mzunguko mmoja unaweza chukua ndoo zile ndogo 5-8!inategemeana na ukubwa wa ile machine(crusher )na inaweza zidi pia kidogo. So unga ni mwingi kiukwel. Sasa vibarua ni hela ya kula tu..mayb uombe uoperator na mkubaliane mlipane mkishauza kifusi. Hapo makubaliano ni yenu wewe na mwajiri wako! Bt haizid 500k had kaz kufunga!

Mie nachoamini pia ni bahati! Kuna dogo ndugu yangu alifika kule mwaka 2017! Akitokea chuo, alifika hana kitu akaomba kwa mzee 200k! Leo hii kila miezi miwili ana faida ya kuanzia 6-8m!so alianza na , 200k akinunua mawe ya bei ya chini(fello) akapanda had kumiliki crusher! Means akianza leo 14th kazi anafunga 14 July anauza kifusi yy hana mpango na plant kbs.faida ndo hizo 6-8m! Ikigoma sana 4m. Kule naona wasomi kama wanatoka mapema eti! Mradi uwe serious na usmart fulani!

Na ukitaka kufanikiwa mapema nenda kwenye mgodi ulolipuka. Sio mgodi uliodormant!

Reactions

Post a Comment

0 Comments