Ili kupunguza tatizo la ajira nchini, serikali kupitia Halmashauri zote nchini na Mfuko wa Rais, wanatoa mikopo isiyo na riba kwa vijana, wanawake na walemavu
Halmashauri zinatoa asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwa vijana, wanawake na walemavu, ikiwa ni asilia 4, wanawake, asilimia 4 vijana na asilimia 2 walemavu
Masharti sina shaka nayo kwa sababu kwa namna moja au nyingine yanafanana na taasisi nyingine za mikopo.
Mfuko wa Rais (PTF) pia unatoa mikopo kwa vijana, ila hawa wamelenga zaidi kwa vijana wanaotoka VETA.
Hii yote ni kupunguza tatizo la ajira nchini, lakini naona vijana na wanawake wana ufahamu zaidi kuhusu mikopo inayotolewa na FINCA, PRIDE, nk. Mikopo ambayo imekuwa mwiba kwa watu wengi kwa kuwa na riba kubwa na muda mdogo wa kurudisha mikopo hiyo
Pia watu wamepoteza vitu vyao kwa kujihusisha na mikopo hiyo. Lakini ikumbukwe serikali inasisitiza vijana wajiajiri, lakini nawaona hawafanyi marketing kiasi cha kutosha ili vijana waweze kujiajiri
Soon nitakuja na suggestion ya kitu gani kibadilishe kwenye mikopo hiyo ili kuwafiki wengi na kuwa na tija kwa vijana walio wengi ambao wana mawazo ya biashara lakini, hawana mitaji ya kuweza kujiajiri
Lakini watu wengi wamekuwa wakitafuta mikopo katika mashirika binafsi yenye riba kubwa, ambayo hata ukusanyaji wake umewafanya watu hao kuwa masikini zaidi kama tafiti mbalimbali zinavyoonyesha
Biashara matangazo, serikali sio kama inafanya biashara lakini kama ina nia ya kuwaokoa vijana na wanawake kwenye mambo ya kujiajiri inaonyesha wazi utangaziji wao hauko sawa na mashirika binafsi ya kutoa mikopo
Nini cha kufanya ili upate mkopo huu?
Nini cha kufanya ili upate mkopo huu?
Jambo la muhimu andaa kikundi Cha watu wasiopungua watano wanaweza kuwa wanawake kwa wanaume au wanawake tu au wanaume tu.
Pili Andika muhutasari wa kikundi kwamba wanachama wameridhia kusajili kikundi Chao
Akikisha kikundi kina katiba ikionyesha idadi ya wanachama, eneo wanapofanyia shughuli zao, uongozi kuanzia mwenyekiti na katibu, namba za simu za viongozi na mengine.
Andika barua ya kuomba kusajiliwa kwa kikundi kwenda kwa mkurugenzi wa Halmashauri usika Ila kupitia kwa mtendaji wa kata usika ili athibitishe uwepo wa icho kikundi usika.
Baada ya kukamilisha hzo nyaraka zote Yani katiba ya kikundi, muhutasari wa kikao Cha wanakikundi wakipendekeza kusajili kikundi Chao pamoja na barua ya kuomba usajili wa kikundi nenda Halmashauri ofisi ya maendeleo ya jamii ukiwa na hzo nyaraka watakupa kimemo uende kilipia elfu kumi Kama sio ishirini kwenye ofisi ya muhasibu mapato ukisha lipiwa nakupewa risti utaludi Tena ofisi ya maendeleo jamii ukiwa na hyo risti uliyo lipia then watakupa hati ha usajili wa kikundi.
Ukisha sajili kikundi Sasa unaweza kuomba mkopo kwa kumuandikia mkurugenzi wa Wilaya barua ya kuomba mkopo ikitaja kiasi na namba ya utambulisho au usajili wa kikundi ambatanisha pia muhutasari wa kikundi wa kinuia kuomba mkopo pamoja na katiba ya kikundi Kisha zipeleke masijala ya mkurugenzi wa wilaya alafu utasubili majibu.
0 Comments