
ALIYEKUWA straika wa Yanga, Mganda Juma Balinya ambaye amevunjiwa mkataba na klabu hiyo, ameweka wazi kwamba amekubali kuondoka ndani ya kikosi hicho baada ya kutemwa lakini anaamini ipo siku atarejea.
Balinya aliyetua Yanga msimu huu akitokea Polisi ya Uganda, amevunjiwa mkataba na anakuwa mchezaji wa pili wa kigeni kuondoka msimu huu baada ya Sadney Urikhob raia wa Namibia.Straika huyo ambaye msimu uliopita akiwa Uganda alifunga mabao 19, amesema anawashukuru Yanga kwa muda ambao amekaa ndani ya klabu hiyo ambapo anaamini baadaye atakuja kurudi ndani ya klabu hiyo.
“Asanteni Yanga kwa muda wote ambao nimekaa ndani ya klabu, naondoka lakini huu ndiyo mpira, siwezi kusema zaidi juu ya kile kilichochukuliwa, natarajia kurudi siku moja hapa,” alisema Balinya.
Social Plugin