Ad Code

Responsive Advertisement

Chuchu Hansy Atoa Sababu za Kumkwepa Ray




Msanii wa filamu nchini Chuchu Hansy, ameeleza kwanini huwa anakwepa maswali ambayo yanamhusu mpenzi wake na Baba wa mtoto wake, Vincent Kigosi ama Ray.



Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Chuchu Hansy amesema huwa anaogopa kwa sababu anajua kuna kuachana na hataki mwanaye akiwa mkubwa, aone akiwa anaongelea mambo hayo.
"Sipendi sana maisha yangu yawe wazi, hata kama ni msanii nataka niwe na mipaka kwa sababu mimi ni Mama mwenye watoto na hivi vitu vinaishi, kunakugombana, kupatana naweza nikaongea halafu kesho mwanangu anakuwa mkubwa anaangalia interview anaona, kwahiyo sina na siishi maisha hayo" amesema Chuchu Hansy.



Pia Chuchu Hansy amezungumzia suala la kutoishi pamoja na Ray, licha ya kuwa ni wazazi wa mtoto mmoja.
"Sidhani kama inawasaidia sana mimi nahisi wangetaka sana kazi kwasababu sisi tumemiss sana kuonekana kwenye game, kwahiyo wangehitaji mambo ya kazi sio maisha yetu binafsi, kwa sababu iwe tunaishi au hatuishi pamoja ni maamuzi yetu na maisha yetu ambayo tumeamua tuishi"ameeleza.
Reactions