Ad Code

Responsive Advertisement

JPM Asajili laini Yake ya Simu Kwa alama za Vidole, Aongeza Siku 20



Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo Desemba 27, 2019 amefanya usajili wa laini yake ya simu kwa kutumia alama za vidole Chato Mjini katika Mkoa wa Geita na kuwasisitiza Watanzania wahakikishe laini zao za simu zinasajiliwa kwa alama za vidole kama ilivyoelekezwa na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA).

Rais ameongeza siku 20 kuanzia tarehe 01 Januari, 2020 hadi tarehe 20 Januari, 2020 kwa wote ambao watashindwa kusajili laini zao katika kipindi cha kuishia tarehe 31 Desemba, 2019 kama ilivyotangazwa na TCRA.

Reactions