Kocha wa Leicester City Brendan Rodger anaamini itakuwa ni vigumu kuwazuia Liverpool kushinda ubingwa wa ligi kuu msimu huu.
Rodgers ameongea hayo baada ya kupokea kipigo cha 4-0 kutoka kwa majogoo hao ambao wamepaa kileleni kwa tofauti ya pointi 13 huku wakiwa na mechi moja mkononi.
“Wanaenda kuwa wagumu sana, sana kuwazuia msimu huu. Timu nzuri, kujiamini kupo juu pia” Rodgers aliwaambia waandishi wa habari.
“Wamekuwa washindi sasa na hawajapoteza mechi nyingi katika kipindi cha miezi 18, wana wachezaji wazuri sasa, uzoefu wa kutosha na ubora wa kutosha kubaki makini na kumaliza kazi” amesema.
Magoli mawili ya Firmino, penati ya James Milner na goli la Alexander-Arnold yanawapa Liverpool ushindi wa 17 katika mechi ya 18 katika safari yao ya kunyanyua ubingwa wa Ligi kuu nchini England.

Social Plugin