
Wizara ya mambo ya nje ya Korea Kaskazini imeikosoa Marekani kama ''mjinga'' baada ya kuitisha mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutokana na kuongezeka wasiwasi kuhusu maroketi ya masafa mafupi yaliyorushwa na nchi hiyo.
Jana Marekani ilisema katika mkutano huo kwamba majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini yanatishia kuufunga mlango kwa matarajio ya kujadili amani.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Korea Kaskazini amesema kwa kuandaa mkutano huo, Marekani imefanya kitendo cha kipumbavu ambacho kitaongeza nguvu yake na kuisaidia Korea Kaskazini kuamua kuhusu kile wanachokichagua.
Rais wa Marekani, Donald Trump tayari amekutana mara tatu na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un kujadiliana kuhusu mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini, lakini nchi hiyo inataka mpango kamili ambao utajumuisha nafuu ya vikwazo.
Social Plugin