
SAMWELY Kisinga, mjasiriamali na mkazi wa Songea ameibuka kidedea kwenye Shindano la Mama Kasema lililokuwa chini ya kampuni ya kizawa ya Nala iliyo chini ya Benjamin Fernandes.
Kisinga alishinda Sh milioni 10 baada ya kuwazidi washiriki wenzake 20 alioingia nao kwenye fainali iliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam kwa kuwasilisha wazo la biashara linalotatua matatizo ya mazingira kwa kutumia takataka kuzalisha sheet za dari (Ceiling board) na mapambo ya gypsum.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika Ofisi za Global Group zilizopo Sinza Mori wakati wa makabidhiano ya zawadi hiyo, Fernandes alisema kuwa anajivunia kuwapa mafunzo Watanzania ambao wamepokea mpango wake kwa ukaribu.

“Sisi vijana tunafanya kazi katika mazingira magumu na licha ya kuwa kampuni yetu ya Nala imepata tuzo nyingi kubwa ila inatambua changamoto za biashara jambo ambalo limetufanya turudishe tunachokipata kwa jamii na Samwely anastahili pongezi kwa kushiriki na kushinda wengine wasikate tamaa,” alisema.
Social Plugin