
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amekubali kujiuzulu kwa askofu mkuu Luigi Ventura, aliyekuwa balozi wa Vatican nchini Ufaransa.
Askofu huyo anakabiliwa na tuhuma za unyanyasaji kingono. Wiki iliyopita Ventura alitimiza miaka 75, ikiwa ndio umri maaskofu wote wanalazimika kuwasilisha maombi ya kujiuzulu kwa Papa.
Francis wakati mwingine huyakubali maombi hayo haraka kama ilivyo kwa Ventura na wakati mwingine huwabakisha watu katika kazi zao kwa muda mrefu.
Mamlaka za Ufaransa zilianzisha uchunguzi dhidi ya Ventura mnamo mwezi Januari, baada ya afisa mmoja mdogo kumtuhumu kwa unyanyasaji.
Vatican ilimuondolea hadhi ya kidiplomasia askofu Ventura mwezi Julai ili aweze kuhojiwa na waendesha mashitaka.
Social Plugin