Ad Code

Responsive Advertisement

RIHANNA AENDELEA KUTENGENEZA MKWANJA MWINGI ZAIDU NJE NA MUZIKI


Licha ya kuwa kimya kwa muda mrefu kwenye muziki, Mwanamuziki Rihanna amegeukia zaidi kwenye upande wa biashara, Riri ameripotiwa kuuza haki za filamu fupi (short film) ya maisha yake kwa mtandao wa Amazon.

Tovuti ya Hollywood Reporter imesema kwamba Rihanna amelipwa zaidi ya Bilioni 57 za Kitanzania kupitia short film hiyo. 
Filamu hiyo ambayo inatayarishwa na director Peter Berg bado haijapewa jina.

Kupitia filamu hiyo utapata nafasi ya kuona maisha ya Rihanna kuanzia muziki, kazi, familia, mapenzi na masuala mengine ya kijamii.
Reactions