
Rais Donald Trump ameukosoa uchunguzi unaokaribia kufanyika kwa barua ya hasira kwa afisa wa ngazi ya juu wa Democrat Spika Nancy Pelosi, akimtuhumu kwa kutangaza accusing her "vita vya wazi dhidi ua demokrasia ya Marekani".
"Umeshushia hadhi umuhimu wa neno mabaya sana ,Uchunguzi!" aliandika katika barua iliyotumwa Jumanne.
Bwana Trump anakabiliwa na kura ya uchunguzi Jumatano kuhusu madai kwamba aliishinikiza ukraine kwa ajili ya maslahi binafsi za kisiasa.
Anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi, utakaoandaa kesi katika bunge la Senati.
Huku kukiwa na matumaini kidogo ya kubadili matokeo ya kura ya uchunguzi huo Jumatano katika bunge, Bwana Trump alitumia barua yake ya kurasa sita kuonyesha hasira yake dhidi ya mchakato na kumpinga Bi Pelosi , ambaye ni Spika wa bunge anaetoka katika chama cha Democratic.
Ilikua ni hatua isiyo ya kawaida ya uingiliaji kati iliyochukuliwa na rais , ambae alipigana kuzuia mchakato wa kumchunguza kwa kuwazuia washirika muhimu kutoa ushahidi katika Bunge la wawakilishi.
Bwana Trump anadai katika barua yake kwamba alizuia "alinyimwa haki ya kimsingi ya kikatiba kuanzia mwanzoni mwa mchakato wa uchunguzi " na "kunyimwa haki za kimsingi zinazotolewa na katiba , mkiwemo haki ya kuwasilisha ushahidi ".
"Haki ya mchakato ilitolewa zaidi kwa wale walioshitaki katika kesi ya Salem Witch Trials," aliandika.
Ukweli ni kwamba rais alialikwa wazi na mwenyekiti wa Kamati ya Sheria ya Bunge kutoka chama cha Democratic kutoa ushahidi katika mchakato wa uchunguzi huo, jambo ambalo lingeruhusu timu yake ya kisheria kuwahoji mashahidi, lakini alikataa.
Meya wa Salem, Kim Driscoll, alituma ujumbe wa Twitter kwamba rais anapaswa "Kujifunza historia," akisema kuwa kesi za kichawi zilizowapata na hatia wahusika zilifanyika wakati hakuna ushahidi, huku kesidhidi ya rais ikiwa na "ushahidi wa kutosha".
CC:BBC
Social Plugin