Ad Code

Responsive Advertisement

Ufaransa: Wafanyakazi wa reli watishia kugoma hadi Krismasi



Chama kikubwa cha wafanyakazi katika usafiri wa reli nchini Ufaransa kimetishia kwamba mgomo wao wa kupinga mageuzi ya malipo ya uzeeni ya Rais Emmanuel Macron unaweza kuendelea hadi katika msimu wa sikukuu ya Krismasi.

Mkuu wa chama hicho, Laurent Brun ameliambia Shirika la utangazaji la Ufaransa, kuwa hakutakuwa na makubaliano ya Krismasi hadi hapo serikali itakapozinduka kabla ya hapo.

Brun amesema itakuwa ni vyema kwa mtu kuwa na siku chache, wiki chache za wakati mgumu, kuliko kuwa na maisha ya shida.

Matamshi ya Brun yametolewa siku moja baada ya Waziri Mkuu wa Ufaransa, Edouard Philippe kutangaza mageuzi kuhusu mfumo wa akiba ya uzeeni, hali inayovifanya vyama vya wafanyakazi vyenye msimamo wa wastani kuunga mkono wito wa viongozi wa vyama vikubwa vya wafanyakazi kushiriki katika maandamano na mgomo siku ya Jumanne.


Reactions