
TAKUKURU mkoani Dodoma inatarajia kumfikisha Mahakamani James Kwangulija, mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu wa Shahada ya Kwanza ya Ualimu Chuo Kikuu cha St. John, kwa kosa la kutoa hongo ya Tsh. 900,000 kwa Msimamizi wa Mitihani ili aongezewe ufaulu wake na wenzake sita.
James ametenda makosa hayo Kinyume cha kifungu cha 15 (1)b cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Sura ya 329, Marejeo ya 2018.
Akizungumza leo Januari 7, 2020, Mkuu wa TAKUKURU Mkoani humo, Sosthenes Kibwengo, amesema uwepo wa tabia ya baadhi ya wanafunzi kutoa rushwa katika masomo unapelekea kuzalisha wasomi wengi wasiokuwa na uelewa katika Taaluma zao, hivyo kutokuwa na sifa za kuajiriwa kwenye soko la ajira hapa Nchini.
Social Plugin