
MAELFU ya waombolezaji wamekusanyika mitaani nchini Iran ili kuomboleza kifo cha Jenerali Qasem Soleimani aliyeuawa na Jeshi la Marekani katika shambulizi la anga wiki iliyopita huku waombolezaji wakijipiga vifua na kuimba “Kifo kwa Marekani”.
Soleimani alikuwa kiongozi wa Jeshi la Iran ambaye alikuwa na ushawishi mkubwa katika nchi za Mashariki ya Kati na alikuwa anatambuliwa kama mtu wa pili anayeheshimika zaidi katika nchi yake.

Mauaji yake yameleta uhasama mkubwa kati ya Iran na Marekani. Iran imetenga kiasi cha ($80m) sawa na Bilioni 184 za Kitanzania kwa mwananchi yeyote nchini Iran ambaye ataleta kichwa cha Rais wa Marekani Donald Trump.
Kwa mujibu wa The News Site, imeripotiwa kuwa pesa hiyo ambayo itachangishwa na wananchi wenyewe milioni 80 wa taifa hilo kila mmoja atachangia dola 1 na jumla ya kiasi kitakachopatikana atapewa mtu huyo ambaye atafanikiwa kuleta kichwa cha Trump.

Hii imekuja baada ya Marekani kutangaza kuhusika kwenye mauaji ya Jenerali Qasem Soleimani, kiongozi wa kikosi maalum cha jeshi la ulinzi wa Iran nje ya nchi kinachofahamika kama Quds.

Social Plugin