Ad Code

Responsive Advertisement

Msolla: Tunashusha Mashine Mbili za Kufunga Kazi



DIRISHA la usajili kueleka Ligi ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (RBA), limefunguliwa rasmi jana huku klabu zote husika kupewa fursa ya kukaa meza moja kuingia mikataba na wachezaji wa kimataifa wasiozidi watano.

Emesu Okare, huyu ni Rais wa Chama cha Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BD) ambaye alizungumza na Gaazeti la Championi jana na kuweka wazi kuwa, dirisha hilo la usajili litafungwa wiki moja kabla ya kuanza kwa mtifuano wa RBA mwezi ujao.

“RBA itaanza rasmi wiki ya mwisho ya Februari ambapo usajili tutafunga wiki moja kabla ya ligi hiyo kuanza, kuhusu wachezaji wa kimataifa ni watano lakini watatu pekee ndio watacheza katika kila mechi na sio wote kwa pamoja,” alisema Okare.

Tayari minong’ono imeanza kusikika juu ya ujio wa staa wa kikapu raia wa Tanzania anayeitumikia klabu ya Betway Power ya nchini Uganda, Amini Mkosa akidaiwa kurudi nyumbani kipindi hiki cha usajili ili timu yake ya awali ambayo ni Savio, imtupie jicho kueleka kivumbi cha RBA.
Reactions