Mahakama yaamuru Netflix kufuta filamu inayoonyesha Yesu kama mtu anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja
Jaji huko Brazil ameamuru Netflix iache kuonyesha filamu "ya kufuru" ambayo inaonyesha Yesu kama mtu shoga
Jaji Benedicto Abicair alitoa uamuzi huo katika kujibu ombi la shirika la Katoliki la Brazil ambalo lilisema kwamba filamu ya The Temptation Of Christ imeumiza "heshima ya mamilioni ya Wakatoliki".
Uamuzi huo wa mahakama ni halali hadi mahakama nyingine itoe amri nyingine tofauti na hiyo.
Filamu inaonyesha Yesu anarudi nyumbani siku ya kuzaliwa akiwa na miaka 30 na anaonyesha ni mtu wa kufanya mapenzi ya jinsia moja.
Social Plugin