Ad Code

Responsive Advertisement

KENYA: MWENYE NYUMBA AMUUA MPANGAJI KWA KUSHINDWA KULIPA KODI YA MWEZI JANUARI



Mwenye nyumba Ngángá Gitau, amemchoma visu mpangaji wake hadi kufa Warren Jirongo (26) baada ya kushindwa kulipa kodi ya mwezi Januari

Wakazi wa eneo hilo wamemzonga mwenye nyumba huyo kwa hasira na kuchoma nyumba zake moto baada ya yeye kumuua kijana huyo

Kijana huyo ni yatima ambaye alikuwa anafanya kazi ya kukusanya uchafu majumbani. Majirani zake wamemsifu kama kijana anayejituma kwenye kujitafutia riziki

Wakazi hao waliingia mitaani na silaha kumtafuta mwenye nyumba huyo ambaye alikuwa amejificha, Polisi walifika eneo la tukio na kuwasambaratishwa raia hao japo uharibifu ulikuwa tayari umeshafanyika.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha mji huku uchunguzi juu ya kifo chake ukiendelea

CHANZO: TUKO
Reactions