Ad Code

Responsive Advertisement

Mamlaka nchini Zambia zinalishikilia gari la kifahari aina ya Bugatti Veyron lililoingizwa nchini humo


Mamlaka nchini Zambia zinalishikilia gari la kifahari, Bugatti Veyron lililoingizwa nchini humo Februari 24 kupisha uchunguzi ili kujiridhisha kama ununuzi wake haujakiuka sheria ya utakatishaji fedha. Hatua hiyo imechukuliwa baada ya gari hilo pekee nchini humo kuibua mjadala.
Mjadala huo mkubwa umeibuka nchini Zambia kufuatia mtu mmoja ambaye hajafahamika kununua gari la kifahari aina ya Bugatti Veyron (TZS 4.6B-6.9B) lililoingizwa nchini humo kwa ndege ya kibiashara. Mjadala huo umechochewa na baadhi ya watu nchini humo kutokuwa na chakula cha kutosha.


Reactions

Post a Comment

0 Comments