Ad Code

Responsive Advertisement

Timu zinazo shiriki ligi kuu nchini Uingereza (EPL) leo zimepiga kura zikitaka dirisha la usajili la majira ya joto lifungwe usiku wa kuamkia Septemba

Timu za Epl Zapiga Kura Dirisha la Kiangazi lifungwe Septemba
Timu zinazo shiriki ligi kuu nchini Uingereza (EPL) leo zimepiga kura zikitaka dirisha la usajili la majira ya joto lifungwe usiku wa kuamkia Septemba mosi kama sehemu nyingine barani Ulaya.
Uingereza waliweka utaratibu kuwa dirisha lao la usajili la majira ya joto linafungwa siku moja kabla ya kuanza kwa ligi wakati sehemu nyingine linakuwa bado lipo wazi.
Ligi za Hispania, Ujerumani, Italia, Ufaransa dirisha lao la usajili la majira ya joto hufungwa Septemba mosi hivyo walikuwa wana uwezo wa kusajili mchezaji kutoka Uingereza wakati dirisha likiwa limefungwa katikati ya mwezi Agosti.
Baada ya kura hizo zilizpopigwa leo kuna uwezekano mkubwa wa dirisha liljalo la majira ya joto likafungwa usiku wa kuamkia Septemba mosi.
Reactions