Mwanaume mmoja (35) ameshambuliwa na panga baada ya kukutwa akifanya mapenzi na Mama yake mzazi mwenye umri wa miaka 55
Majirani wa familia hiyo wamesema Kijana huyo amekuwa akifanya kitendo hicho na Mama yake kwa muda mrefu na jambo hilo halikuwa siri
Siku ya tukio, Mdogo wa Marehemu alienda kumuangalia Mama yake na alisikia watu wakiongea ndani lakini alipojaribu kumuita hakuna aliyejibu, na akaamua kuvunja dirisha. Alikuwakuta Kaka yake na Mama yao kitandani huku wakiwa wamelewa
Baada ya kufumaniwa, Marehemu alijaribu kukimbia lakini mdogo wake alimshambulia na panga na kumjeruhi vibaya. Polisi walifika eneo hilo masaa matatu baadaye na kukuta ameshafariki
Dada wa Marehemu amesema Kaka yake hakuwa ameoa na alikuwa na tabia ya kukaa nyumbani kwa Mama yao nyakati za usiku. Baba yao yupo Nairobi kikazi na hajarudi nyumbani kwa miezi miwili sasa
Mama huyo anashikiliwa na Polisi na aliyemuua ndugu yake bado hajakamatwa

0 Comments