Ad Code

Responsive Advertisement

SHERIA ZA SOKA ZA FIFA: FAHAMU SHERIA NAMBA 3 INAYOHUSU IDADI YA WACHEZAJI


Kwa mujibu wa Sheria za FIFA (Shirikisho la Soka Duniani) mwaka 2015/16, mechi inachezwa na timu mbili, kila moja ikiwa na Wachezaji wasiozidi 11, mmoja wao ni Kipa. Mechi haiwezi kuanza ikiwa timu yoyote ina Wachezaji chini ya 7

Kiwango cha juu cha kubadili Wachezaji wakati wa mechi kwenye mashindano rasmi yaliyoandaliwa na FIFA au Wanachama wake ni Wachezaji watatu. Kanuni za shindano husika zitaeleza wachezaji wangapi wakae benchi kuanzia 3 hadi 12 

Kwenye mashindano mengine (Kitaifa) hadi Wachezaji 6 wanaweza kubadilishwa lakini kwenye mashindano mengine Wachezaji zaidi wanaweza kubadilishwa

Katika mashindano ambayo zaidi ya Wachezaji 6 wanaweza kubadilishwa, timu lazima zikubaliane na Mwamuzi wa mchezo aambiwe. Hayao yasipofanyika Wachezaji 6 wanaweza kubadilishwa

Kurudishwa Uwanjani kwa mchezaji aliyefanyiwa mabadiliko kunaruhusiwa tu kwenye mashindano ya viwango vya chini au mashindano kwa ajili tu ya burudani lakini lazima wanaohusika wakubaliane

Mchezaji yeyote anaweza kubadilishana nafasi na Golikipa ilimradi tu, Mwamuzi apewe taarifa kabla na ubadilishanaji huko kufanyika mpira ukiwa umesimama

Mchezaji aliyepewa kadi nyekundu kabla ya mpira kuanza, nafasi yake inaweza kuchukuliwa na mchezaji yeyote aliye benchi ila haiwezekani mchezaji mwingine kuingia ikiwa mchezaji atapeka kadi nyekundu mchezo ukiwa umeanza


Reactions

Post a Comment

0 Comments